Kutuhusu

BCIC Maji Meupe (Biblical Counselling and Intercession centre) ni kanisa lililo chini ya Wapo Mission International linalotoa maombi na ushauri wa kibiblia ili kuleta mabadiliko kwenye jamii. Shirika letu limesajiliwa nchini Tanzania na linatambulika na vyombo vya dola na mashirika mbalimbali. Pia linaendesha vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Wapo Radio FM 98.1, Wapo TV, gazeti msemakweli na shule Shalom Pre and Primary School.
Kanisa la BCIC maji meupe limejikita kuwahudumia watu kutatua matatizo ya kiuchumi, kiafya, kifamilia, kiroho na kijamii kwa misingi ya neno la Mungu (Bibilia).

Tunaamini

Mungu anaweza kufanya Mambo Yote.

Kauli Mbiu

Hakuna lisilowezekana kwa Mungu

Lengo

Tunataka kusambaza neno la Mungu pande zote za Dunia.